Miaka Kumi na tatu ya Moto wa Uamsho.

tunamtaka BWANA na Nguvu zake.

Kuhusu TAG
tag logo

Kuhusu

Idara yetu

Christian Men’s Fellowship (CMF) una historia ndefu katika TAG. Kwanza, wazo lilianza kama shauku ya uongozi wa Kanisa kitaifa, Pili, ilitokana na hitaji la wanaume wenyewe, na vilevile lilikuwa ombi la muda mrefu kutoka kwa Idara ya Wanawake Watumishi wa Kristo (W.W.K) wa kanisa letu. Mwaka 2008, wakati wa awamu ya tatu ya uongozi wa kanisa chini ya Askofu Dr. Barnabas Mtokambali, TAG ilitengeneza Dira ya Maendeleo ya Kanisa ya utekelezaji wa miaka kumi ya mavuno. Katika Eneo C linalosema “Inua viwango vya Ibada ya binafsi na pamoja”, kipengele cha C4:5-kina mkakati unaosema, “Anzisha Idara ya Wanaume”. Ili kutekeleza azimio hili, uongozi wa TAG ulifanya maandalizi yafuatayo:-...
Kuwaandaa wanaume
Jitihada zilifanyika kuwapata viongozi wa Idara ya Wanaume ya kanisa la Assemblies of God Jimbo la Southern Missouri, Marekani ili kuja Tanzania kutoa semina za uhamasishaji zilizofanyikia kwenye chuo cha Central Bible College (CBC), Dodoma mwaka 2009 na 2010. Idadi kubwa ya wanaume waliohudhuria semina hizi waliazimia kuwa Idara ianzishwe.
Vikao vya Uongozi wa Kanisa
Maono na mapendekezo kuanzisha Idara ya Ushirika wa Wanaume Wakristo yalijadiliwa katika vikao vya uongozi wa kitaifa wa kanisa. Azimio liliwasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya TAG na kupitishwa kwa nia moja. Hatimaye azimio lilipelekwa kwenye Baraza la Waangalizi na Mkutano Mkuu mwezi Agosti 2010 na kupitishwa. Idara hii ilizinduliwa na Uongozi wake wa kitaifa kuteuliwa rasmi katika Mkutano Mkuu wa TAG mwaka 2012.
Mchakato wa Kuandaa Mwongozo
Kamati ya Utendaji ya Kanisa iliteua wajumbe wa Timu Kazi ya kuanzisha mchakato wa Mwongozo huu. Kwa kuzingatia hadidu za rejea, kamati ilifanikisha kazi iliyokusudiwa. Tunamshukuru Mungu kwamba hatimaye Mwongozo ulipatikana na Idara ikaanzishwa.

MAMBO MUHIMU KUHUSU IDARA

CMF

MAONO

Maono ya CMF ni kuona mwanamume aliyerejea katika nafasi yake ya awali ya uumbaji wa Mungu (Mwanzo 3:9) na kufanyika sifa na utukufu wa Kristo ili kutimiza kusudi la Kristo kupitia Kanisa pamoja na malengo ya TAG kitaifa.

DHIMA

CMF ipo ili kuwezesha wanaume kuabudu, kuwa na ushirika, kujengana, kutumika na kufanya uinjilisti.

KUSUDI KUU

Kuwajenga na kuwaunganisha wanaume ambao ni washirika wa TAG ili kukuza umoja na ushirika miongoni mwao na kati yao na Kanisa (Mdo 2:44-47).

Marejeo

Shuhuda

Je! unahitaji msaada zaidi?

+255 685 694 524
tagcmtaifa@gmail.com

tuma hapa

fanikiwa! ujumbe umetufikia.
imefeli! tatizo la kimtandao.